KARIBU KATIKA
Hii ni website ya Kiswahili na English na imebuniwa kwa ajili ya wanafunzi wa Kiingreza wanaotumia Kiswahili, Website hii imedhaminiwa na "Muhraja's après ski and Nocturnal English Program" iliyopo mtaa wa Yombo Temeke Chang'ombe inayofundisha tuishen ya kiingereza kila na usiku kuanzia saa moja hadi saa tatu jioni.
Madhumuni makubwa ya home page hii ni kukuza uwezo wa kupata msamiati na mambo mengine muhimu kwa mwanafunzi anayeanza kujifunza Kiingereza, Kwa wanafunzi ambao wanajua Kiswahili lakini hawajui Kiingereza natumaini sasa watapata wepesi kiasi fulani kujisomea na kujifunza Lugha hii ya Kiingereza kwa kutumia homepage hii. Malengo maalum yaliyomo ni katika kumsaidia mwanafunzi anayetumia Lugha ya Kiswahili katika kujifunza lugha ya Kiingereza na pia anaye tumia lugha ya Kiingereza katika kujifunza Kiswahili, Amma hii "website" itamsaidia pia mwanafunzi aweze kuelewa masomo yake vizuri shuleni kwa kuwa Kiingereza ndicho kinapotumika hasa Tanzania na Afrika ya mashariki. Katika homepage hii yapo majina ya vitu ambayo nimeona ni bora kuyawekea picha katika kuyaeleza kutokana na kushindwa kuyaweka bayana katika lugha ya Kiswahili, kwa kuwa dhumuni langu ni kueleweka basi si vibaya nikitumia picha (taswira hizo) pale nitakapoona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.Naomba sana watembeleaji wa "website" hii watumie nafasi hii katika kuisoma na kuielewa na kutoa mawazo yao katika kuiendeleza ili iweze kutoa huduma ya hali ya juu kuliko ilivyo sasa.
Kuhusu mimi ni kuwa, nimekuwa nikisomesha English kama mwalimu wa madrasa za kiislamu, nilikuwa nikifundisha madrasa moja iitwayo "IQRA ISLAMIC CENTRE" ambayo iko mtaa wa Rusende Chang'ombe Temeke, nilikuwa nikifundisha hapo tangu mwaka 1997 hadi 1988 ambapo tukaanzisha pamoja na wenzangu madrasa iliyojulikana kwa jina la "ISTIQAAMA ISLAMIC EDUCATION CENTRE" iliyo kuwepo katika mtaa wa Uzuri jirani kidogo na madrasa ya kwanza, (Yaani "Iqra Islamic centre") nilifundisha hapo kuanzia mwaka huo hadi mwaka 2000 ambapo nilipoanza masomo ya matengenezo ya Computer ninayo endelea nayo hadi sasa. Ingawa nimekuwa nikisoma masomo haya, bado nimekuwa nikiendesha masomo ya "tuition" jioni baada ya masomo yangu. Tuishen hii naifanyia nyumbani na inajulikana kama "muhraja's Après ski and Nocturnal English program kwa kuwa yenyewe ni ya jioni sana na usiku.
Katika kufundisha muda wote huo wa kufundisha niliweza kujua matatizo mengi wanayo yapata wanafunzi katika kusoma somo la Kiingereza, ninataraji kurahisisha njia ya kusoma kwao katika "site" hii.
Kutokana na matatizo yanayo wakabili wanafunzi katika kujifunza Lugha ya Kiingereza ambayo nimeyakuta wakati wa kuwasomesha, nitajaribu kuyaweka wazi tu baadhi ya kwa muhtasar, lakini kwanza kabisa nieleweke kuwa hii "site" sio ya wanafunzi wa shule peke yao, kwa hiyo nitaanza kuandika mambo muhimu hata kwa yule ambaye ndio anaanza kujifunza mwenyewe aweze kufaidika.
Tunaanza moja kwa moja na somo letu bila kupoteza wakati. Kwa kawaida tunajua kuwa kila lugha ina fasaha yake, na lafidh yake. Lakini yote hayo yatakuja baadaye tukijaaliwa, katika mambo tunayo takiwa tuyajue kwa sasa ni vema tukijua salaam. Katika lugha tunayoisoma, vipi tusalimie asubuhi, jioni na usiku.
Kwa Kiswahili: tunapofikiwa na asubuhi tuna wajulia watu hali kwa kusema "Umeamkaje" au "Habari za asubuhi" kwa mchana tunasema "Umeshindaje?' au "Habari za mchana " ambapo kwa Kiingereza tunapo wajulia watu hali tunasema kwa wakati wowote "How are you?" inatamkwa kwa kiswahili kama (Haw -a yuu?)
Lakini katika Kiswahili kuna utaratibu kutokana na mazingira na utamaduni, Vile vile katika Kiingereza kuna utamaduni wa Waingereza katika masuaIa mengine ya kilugha na utaratibu wa kusalimiana. Nitaangalia yale yanayo weza kuingiliana na kuyaandika humu. Kwa kawaida ukisalimiana na mtu kwa Lugha ya Kiswahili ikiwa ni mkubwa utamwamkia kwa kusema "shikamoo", naye ataitika "Marhaba" na kisha utamuuliza au atakuuliza "Umeshindaje" au "Umeamkaje" la kwa mtu mzima kama wewe ni mdogo kwake huwezi kumuambia mtu mzima "umeshindaje" moja kwa moja bila kummwamkia "Shikamoo" au"umeamkaje" bila kuanza kumsalimia kwa kusema "Shikamoo!" Hii ni kutokana na maadili ya jamii inayotumia lugha hii.
Amma kwa Kiingereza tunaweza kusalimiana kwa kusema "Good morning" (Gud moning") ikiwa ni asubuhi au "Good afternoon" (Gud afta nuun) ikiwa ni mchana na "Good evening" (Guud ivining) ikiwa ni jioni na baada ya kutoa salamu moja wapo katika hizi inayoendana na wakati ulio nao kisha utamjulia hali uliyempa salamu kwa kumuuliza "How are you?" (haw a yuu)
N.B: Maandishi kwenye mabano yanaonyesha namna gani msomaji wa Kiswahili atakavyo soma na kutamka maneno yaliyo andikwa pembeni ya mabano hayo.
Amma kwa wale wanaojua Kiswahili kizuri, ambacho kwa sasa watu wengi wamekuwa hawatumii salamu hizi ambazo ningesema ndio hasa hutafsiri maneno "Good morning" "Good afternoon" na "Good evening"
"Good morning" hutafsirika kwa Kiswahili sahihi ni "Sabalkheri" (Neno la Kiswahili lililokopeshwa kutoka kwenye lugha ya Kiarabu likiwa na maana ya "asubuhi yenye kheri". asili ya neno hili ni "Swabaahul khayr" na hivi ndivyo maana ya "Good morning"( Gud moning') ilivyo (literal translation)
kwani msingi wa neno hili ni katika kumtakia mtu asubuhi njema.
Amma kwa mchana tunasema "Masalkheri" hiki ni Kiswahili rasmi, ingawa watu wengine huweza kuona ajabu lakini ndivyo hasa ilivyo, Kiswahili kwa kufundishia Kiingereza yabidi wakati mwingine tutafute Kiswahili kile cha asili ambapo kwa sasa hivi ni aghalabu kukisikia, na hiki ndio Kiswahili rasmi kinachoweza kuendana kwa kiasi kikubwa na maneno hayo ya Kiingereza. Kwani haya maneno yanaashiria kumtakia mtu siku yenye kheri, ambayo kwa Kiingereza ni "Good afternoon" (Hutamkwa kwa Kiswahili kama "Gud afta nuun")
Amma kwa jioni tunasema "good evening" (Gud ivining) hadi pale tunapofikiwa na muda wa kwenda kulala tutasema "good night" (Gud nait)
Kwa ufupi tu, hivi ndivyo itakuwa katika mazungumzo ya watu wawili, mmoja anaitwa Hilali na mwingine anaitwa Canoksan
HILALI: Good morning sir, (gud moning sa)
CANOKSAN: Good morning, how are you? (gud moning' , haw -a- yu?)
HILALI: I am fine, thank you. (ai em fain)
N.B: Neno "Sir" hapo juu maana yake kwa Kiswahili ni "bwana" na hii huitwa mtu wa kiume unayemuheshimu
Amma kwa upande wa wanawake ni "maadam" yaani "bibi" (hii ni bibi ya heshima na sio ile ya uzee)
Katika namna nyingine ya salamu ni kusema "Hello!" na anayesalimiwa atajibu kwa kusema kama alivyo sema mwenzake "Hello!" na kisha wataendelea kuulizana hali na mambo mengine yatafuatia. Hii salamu vile vile inaweza kusikika sana katika mito ya simu na ni maarufu, lakini wakati mwingine huja kwa hali ya kukatishwa, yaani waweza ukakuta mtu akikusalimia kwa kukwambia "Hi!"
Tukirejea Katika mazungumzo hapo juu ya Hilali na rafiki yake (Canoksan) Kuna sentensi "I am fine" maana yake, mimi ni mzima thank you, yaani nashukuru/au ahsante
Katika salamu kama tulivyoona hapo juu kuna "Good morning Sir",
Good morning maadam (kwa mwanamke mheshimiwa), vile vile twaweza kutumia majina hapo chini kuyaongezea mbele yake baada ya kusema "Good morning.........", "Good afternoon..........." au "Good evening........"
Neno matamshi yake maana yake
Father (inatamkwa kwa Kiswahili kama fadha) baba
Mother (inatamkwa kwa Kiswahili kama madha) mama
Sister (inatamkwa kwa kiswahili kama "Sista") dada.
Uncle (inatamkwa kwa kiswahili kama "anko") mjomba au baba mdogo.
Aunt (inatamkwa kwa Kiswahili kama "ant") shangazi au mama mdogo.
Son (inatamkwa kwa Kiswahili kama "san") bin (mtoto wa kiume)
Daughter ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;; kama "douta") binti (mtoto wa kike)
Grandson ;;;;;;;;; ;;;;;;;;;;;;;;kama "grensan") mjukuu (wa kiume.)
Granddaughter ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;kama "gren douta") mjukuu (wa kike).
Grandfather ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;; kama "grendfadha") babu.
Grandmother;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;; kama "grenmadha") bibi.
Nephew ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;; kama "nefiu") binamu.(mtoto wa kiume wa "uncle")
Niece ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;; kama "niis') binamu (mtoto wa kike wa "uncle" )
Grand nephew ;;;;;;;;;;;;;;;;;;; kama "gren nefiu") mtoto wa kike wa binamu.
Grand niece ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;; kama "grend niis") mtoto wa kiume wa binamu.
N.B: Tazama neno "Uncle" hapo juu ili uweze kupata maana ya "nephew" na "niece". Kumbuka kuwa hii ni tofauti na ile ya Kiswahili ambayo wengi tumezoea kuwa mjomba ni kaka yake mama. kwa Kiingereza Uncle ina maana mbili, aweza kuwa ni kaka yake mama au ndugu yake baba. yaani kwa ufupi ina maana ndugu wa kiume wa mmoja wa wazazi wako ndiye huitwa "Uncle" amma kwa upande wa "aunt" ni ndugu wa kike wa mmoja wa wazazi wako.
Amma kwa upande wa salaam tumeshaona zilivyo kwa ufupi, sasa tunakwenda katika kuagana.
Kwa kuagana tunasema kwa Kiingereza "Good bye" na Yule anaye agwa atasema "Bye"
Kiingereza ni miongoni mwa lugha zinazotumiwa na watu wengi duniani. nacho kiingereza kimekuwa na namna mbili kuu, Kiingereza kinachotumika sana Amerika (Marekani/ American English) na Kiingereza kinachotumika sana Uingereza (British English). Usiwe na wasiwasi hata kidogo kwa kuwa tofauti iliyopo haiwezi kukufanya wewe ubabaike katika kujifunza lugha hiyo, kwani tofauti hii siyo ya kufanya wazungumzaji wasielewane, la sivyo, ila tu ni matamshi (Lafidhi)
Namna ya kutamka maneno ya Kiingereza na namna ya Kusoma:(how to read English words)
Hii ni mada miongoni mwa zile nilizodhamiria kuziandika humu katika "website" hii. Nitatumia jitihada yangu nitakayo jaaliwa katika kufikisha mada hii. Katika Lugha ya Kiingereza tunajua kuwa ina lafidh yake, lugha ya Kiarabu, Kijerman, Kisomali, Kidachi, Kiswahili n.k vina lafidh zake kila moja tofauti na nyingine. Kama mtu akiongea Kiswahili kwa lafidh ya Kiingereza atajulikana tu, kadhaalika kwa Lugha ya Kiingereza. Kwanza kabisa kitu cha msingi nitajaribu tu kuonesha namna ya kusoma.
Tunaanza na alfabet za Kiingereza;
Aa Bb Cc Dd Ee Ff Gg Hh
Ii Jj Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv Ww Xx
Yy Zz
Namna ya kuzitamka kwa kutumia lafdhi ya maadishi ya Kiswahili:
A (Ei) B (bii) C (Sii) D (Dii) E (ii) F (Ef) G (Jii) H (ech) I (ai)
J (Jei) L (El) M (Em) N (En) O (o) P (pii) Q (kyu) R (ar) S (Es)
T (Ti) U (yu) V (vi) W (dabli yu) X (Eks) Y (Way) Z (zed)
Ni muhimu sana kujua na kuhifadhi alfabeti hizi kwa kuwa kwa kiasi fulani zaweza kukusaidia katika kusoma Lugha hii. Hapa nitatoa mifano michache tu ya namna ziwezavyo kukusaidia Alfabet hizi;
Mara nyingi tunaweza kuiona herufi "a" ikitumika kabla ya majina ya vitu vinavyohesabika tena ikiwa kitu chenyewe kiko katika hali ya umoja,
Mfano; A boy ( E boy), A stick ( E stik)
A toy ( E toy) A school ( E skul)
Katika mifano mingine ya namna ya kuisoma herufi hiyo ikiwa imefuatana na konsonanti (yaani herufi zote zilizo baki baada ya kuziondoa irabu (a, e, i, o, u):ya kuonyesha kuwa itabaki kuwa katika matamshi ya "e" ni kama ifuatavyo hapo chini; Angalia herufi zilizoandikwa kwa maandishi ya italic na kukolezwa yote yanatamkwa kwa kuwekwa "e" kama ulivyoona hapo chini, na zile zenye kuishia kwa kuandikwa "e" mwishoni haitasomwa ile "e"
A cap, a can, A mat, cat, rat, bat, at, hat, lad, lab, hate, Cake, Date, fate, gate, late, mate, nape, name, page, pane, rate, race, rage, rake, raze, sake, sale, same, sane, save, take, tale, tape, base, bake, bale, lame, bane, paste, lame, compensate, validate, calculate, mandate, defecate, indicate, decade, evaluate, dedicate, manipulate, evaporate, complicate, chase, rain.
N.B; Katika maneno hapo juu yenye herufi "a" na kufuatiwa na konsonant kisha herufi "e" mwishoni kama ulivyoona hapo juu, maneno hayo yote yatatamkwa ile "a" kama "ei" kwa maana hiyo basi, neno "indicate" litatamkwa kama "indikeit", na hii ni kwa sababu herufi "a" katika maneno kama hayo, hutamkwa kama ilivyo tamkwa katika kusoma "alfabet"
Jaribu kuyasoma maneno hayo kwa sauti, yote yana matamshi yenye sheria moja hapo juu,na hutamkwa kwa sauti ya kutoka kwenye kushuka, kupanda na kushuka tena, hii ni kama inavyotamkwa neno la Kiswahili "Kweli"
Tukizidi kuendelea kuona namna gani ya kutamka maneno ya Kiingereza, tujue pia yapo maneno yanayo andikwa yakiwa na herufi "a" mwishoni na ikifuatiwa na herufi mbili, yaani "re" yakawa yanaishia na herufi hizo tatu (yaani ...are") basi herufi hizo zote pamoja zitatamkwa kama "ea"
Kwa maana hiyo basi, mahali pa herufi hizo tatu za mwishoni zitatamkwa kama "ea" kwa matamshi ya Kiswahili, Angalia mifano hapo chini;
bare, rare, fare, care, share, dare, hare, mare, pare, ware, declare, tare, Clare, (mfano wa neno la kwanza ambapo ndivyo yatakavyosomwa mengine ni "Bea" )
Pia yapo baadhi ya maneno mengine ya Kiingereza huchukua sura ya "a" kama ilivyo, yaani hutamkwa hivyohivyo kama "a" Angalia mifano hapo chini;
Data, fat, mama, daddy, bad, Sad, manner, ladle, glass, Class, habit, lack, last, man, human, mad, pass, past, path, patron, papa, sample, salary, vacant
Baadhi ya maneno ya Kiingereza ambayo Kiswahili yawezayo kutamkwa kama "a"na baadhi ya yale yaliyobeba herufi zenye sauti ya a
maneno yaliyo kusanya herufi zinazo simama mara nyingi kama "a" mfano; 'er', "ur", "ar", "or" baadhi ya konsonant zikifuatiwa na ry hugeuza 'y' kusomwa kama "ai"
Mifano katika herufi "er" ni; Teacher, butcher, driver, player na kadhalika
Mifano katika herufi "ur" ni; burn, turn, fur, burry, curry, hurry, turmoil na kadhaalika
Mifano katika herufi "ar" ni; Bark, car, dark, smart, art, start, award, arrive, arm, around na kadhaalika.
Mifano katika herufi hizo ni; Doctor, error, indicator, inductor, terror, conductor, coordinator, na kadhaalika.
Hapa tumechagua yale maneno ambayo mara nyingi huwa yanatamkwa kama "a". kwa hiyo yapo machache sana ambayo yana sifa hizi na yakatamkwa tofauti, lakini hilo usiogope kwa kuwa sio mengi, mfano wa mojawapo katika hayo ni force (hutamkwa kama "fos")
Mfano wa konsonant zikifuatiwa na "ry": ni Try, fry, cry, dry, krypton,
N.B; katika herufi "y" iliyokolezwa hapo kwenye mfano wa mwisho itasomwa kama "ai" na hivyo yatatamkwa maneno yote hapo juu katika sehemu ya "Y"kuwa "ai" (mfano katika neno la mwanzo miongoni mwa mifano hiyo, neno "try" litasomwa kama Trai.
Pia zipo mifano kama hii katika maneno kama "deny", Verify, Specify, vilify, simplify, justify, magnify n.k.
Katika maneno haya, ambayo mara yaliyo mengi sana husomwa kwa kutiwa sauti "ai" sehemu ya "Y" ni yale yanayoishia na "y" iliyo mbele ya na "f"
Tazama mifano hapo chini na usome kwa sauti.
Classify, Simplify, amplify, rectify, fortify, horrify, clarify, testify, signify, notify, identify, electrify, satisfy, sissify.
Ni maneno mengi ya Kiingereza unaweza kukutana nayo yenye kusomwa sehemu iliyo kutana herufi mbili (yaani "al") kama kutamkwa kama "o" inavyotamkwa kwa Kiswahili, baadhi ya maneno kama hayo ni;
All, small, principal, pen pal, sandal, trial, special, typcal, electrical, commercial, legal, national,original.
baadhi ya Maneno ambayo yatasomwa kama "e"( Some of words that will sound as "e" in Swahili)
Maneno hayo yanakusanya herufi ambazo sitasomeka kama "e"; Kwa mfano, "ir", "e", "a', "ai"
Mfano wa maneno hayo yaliyokusanya herufi 'ir" ni kama; Firm, confirm, dirt, skirt, thirty, thirsty, chair, first, third affirm, girl, infirmary, n.k
Mfano wa maneno hayo yaliyokusanya herufi "e" ni kama; elbow, escort, escape, entire, essay, message, end, especially n.k.
Mfano wa maneno hayo yaliyokusanya herufi "a" ni kama; blame, care, take, safe, came, cane, crane, crake, sane drake, flame, lame, name, same, fame, bane, n.k
Mfano wa maneno hayo yaliyokusanya herufi "ai" ni; mail, train, rain, abstain, bargain, again, grain, chain, drain, obtain, cocaine, n.k (N.B: katika herufi hizi "ai" hutamkwa kwa mfumo wa Kiswahili wa "ei" kwa maana hiyo itasomwa neno la kwanza kama "blei m")
Mchanganyiko wa herufi na namna zitakavyotamkwa katika Lugha ya Kiingereza;
Soma kwa sauti maneno yafutayo; (kumbuka kuwa maneno haya ni yale yenye mfumo wa a kutamkwa kama 'e' ya Kiswahili)
Play, tray, pray, May, hay, Okay, hurray, ray, say, day, lay, nay, pay, way, always, away, essay stay, bray, astray, ashtray, always. betray, decay, Monday, Tuesday, Wednesday, Thursday, Friday, Saturday, Sunday, bay.
Zipo herufi nyingine za Kiingereza ambazo zinazoweza kututatanisha ikiwa zitakutanishwa na baadhi ya herufi, mfano wa herufi hizi ni: "ng", nc, th, al, ..ture, ..sion, ..tion, ..uce, konsonant iliyofuatiwa na herufi "le", Ph
Katika herufi tulizoziona hapo juu ni kama ifuatavyo;
'NG' Herufi hizi mara nyingine katika Kiigereza hutamkwa kwa matamshi ya Kiswahili kama vile itamkwavyo katika "Unga" n.k, lakini mara nyingine hutamkwa kama "nj" na wakati mwingine kama "ng'" tunavyo tamka, mfano katika maneno hapo chini
"Danger, stranger, ganger, range, arrange, tangerine, fringe, syringe, angel, na kadhaalika.
Katika mifano ifuatayo hapo chini, herufi hii husomwa kama 'ng' tofauti na hiyo hapo juu ambayo ilisomwa kama 'nj'
Monger, mango, Single, singular, angle, bingo, hanger, hungry,
Mifano mliyoiona hapo juu ni ile ambayo "ng" katika lugha ya Kiingereza hutamkwa kama itamkwavyo "ng" inavyotamkwa katika Kiswahili. Sasa yabidi uwe makini sana, kwani sasa tunaelekea ambapo herufi hizohizo hutamkwa kama ng' inavyotamkwa katika neno "ng'ombe" na hapa yapo maneno mengi sana ya Kiingereza hutamkwa kwa namna hii, ndipo penye maneno mengi kuliko hata hizo mbili tulizo taja hapo juu.
Hutumika katika maneno yanayo ashiria vitendo yanayoishia na ..ing" mfano; Going, reading, n.k tutaona zaidi katika Somo la "verbs" (yaani matendo).
Maneno yaliyo mengi sana kwenye Kiingereza yenye herufi "ng" yanatamkwa kwa sheria hii tuliyoitaja ya matamshi, baadhi ya hayo ni kama tunavyo yaorodhesha hapo chini;
Sing, ring, Song, Bring, Sting, strong, Cling, Spring, Ping, dung, swing na kadhalika.
Yafuatayo ni maneno ambayo herufi "ng" itasomwa kama "nj"
Sponge,
Tunazo herufi ambazo twaweza kukutana nazo katika kozi yetu hii ya Kiingereza kama "nc". Herufi hizi nazo husomwa kwa namna tofauti kama zitakavyo onyeshwa hapo chini na kutolewa mifano.
Kwanza kabisa,herufi hizo hapo juu ("nc") hutamkwa kama "Nk" kwa Kiswahili na pia wakati mwingine hutamkwa kama "ns" na mahali pengine hutamkika kama "nshjy"
Amma kwa upande wa mfano tuliotoa hapo juu wa kwanza ambao tumesema kuwa zitatamkwa kama 'nk'
Ni kama ifuatavyo,
Uncle,
Kwa upande wa mifano katika matamshi ya pili ni kama "permanence, transparence, Commence, appliance, bounce,
Katika Lugha ya Kiingereza neno lenye herufi "th" lina namna mbili katika kutamkwa, namna ya kwanza ni katika kule kutamkwa kama inavyo tamkwa katika lugha ya Kiswahili mfano katika neno kama "thamani", na namna ya pili hutamkwa kama inavyo tamkwa "dh" kama inavyotamkwa katika neno "dhahabu"
Hebu tuone mifano ya maneno ya kutamkwa kwa "dh" na halafu baadaye tuone ya kutamkwa kwa "th"
Ifuatayo ni mifano ya maneno ambayo herufi "th"ya hutamkwa kama "dh"
This hutamkwa kama ("dhis") na ina maana hii/hili/hiki/huyu n.k
Those hutamkwa kama ("dhoz) na ni wingi wa "This"
The hutamkwa kama (dhe) ikiwa ina maana mtu huyo/kitu hicho (Yaani kitu au mtu ambaye/ambacho ameshatajwa/kimeshatajwa na sasa anawakilishwa/kinawakilishwa tu na neno hilo tu.)
That yaani ile/yule/
Those ni wingi wa "that" (yaani wale/...)
Ifuatayo ni mifano ya maneno ambayo herufi "th" hutamkwa kama "th"
thermometer (hili ni jina la kipimo cha kupima joto)
Theology, thermostat, thigh, thing, thought, think, python, marathon, na kadhaalika.
Miongoni mwa maneno ambayo yanavyo andikwa hutamkwa tofauti ni pale tunapokutana na neno lililobeba herufi nne zilizo fuatana pamoja mabazo herufi hizo ni "ture". Herufi kama hizi zinasomwa kwa matamshi ya Kiswahili kama "cha" Angalia mifano ya maneno hayo hapo chini, Isome, kumbuka kuwa kila penye neno "ture" lisome kama "cha"
Picture, culture, mature, nature, expenditure, agriculture, future, puncture, feature,
Matamshi mengine ni kama yale tunayoya soma kwenye herufi kama "sion" na "tion" ambayo yana namna mbili za kusomwa, namna ya kwanza yatasomwa kama "shen" na maneno mengine yatatamkwa kama itamkwavyo "je" katika lugha ya kifaransa" Kwa kiswahili inakuwa ni vigumu kuelezea kwa kuwa hakuna neno la Kiswahili laweza kufananishiwa,ila najaribu tu kulieleza katika kulitamka kama "nshjyen" , basi nitatoa mifano ya namna ya kulitamka kama "shen" na kisha kwa mifano ya namna hiyo ya pili.
Natuanze kwanza na mifano hiyo ya namna ya matamshi ya kwanza ambayo tumesema yatakuwa yanatamkika kama "shen" na kisha tuone mifano ya yale yatakayotamkika kwa Kiswahili kama "shjyen" (Kumbuka kuwa unatakiwa uyatamke bila irabu (vowels) kama yalivyo isipokuwa irabu moja tu ya mwisho iliyofuatana na herufu n")
Nation, ration, congratulation, graduation, inauguration, decision, passion, session, decision, narration, condition, recognition, ignition, abortion, extraction, supplementation, institution, correction, resurrections, Satisfaction, alimentation, monopolization, liberation, celebration, cerebration, documentation, application, reduction, addition, subtraction, Suggestion, animation, session, affection, defection, generation, passion, partition, fumigation, ablution.
Matamshi yote hapo juu ya "sion" na "tion" yatasomeka kama "shen" kwa matamshi ya Kiswahili. Sasa tuone mifano michache ya yale yatakayo tamkwa kwa matamshi ya Kiswahili ya "nshjyen"
Katika matamshi ya "nshjyen" ambayo kwa Kiswahili tulisema hayapo ila hapa tu ni jitihada ya kuyaweka ili mtu atamke kwa kusoma mojamoja kama lilivyo bila irabu, Maneno yanayo tamkwa kwa mtindo huu ni kama yafuatayo ambayo yenyewe yanakusanya mara nyingi herufi kama "nc" na "tia",
Vision, visual, usual. na kadhaalika.
Kwa ujumla na kwa ufupi wa mada tunayoisoma, maneno yanayo somwa kama 'shen' ambayo ndiyo yanaitia hiyo "sh" kwenye "shen" ni haya hapa chini;
Herufi hizi zilizoandikwa kwa italic mahali pengi husomwa kama "sh" katika matamshi ya Kiswahili, tazama mifano ya maneno hayo hapo chini.
Appreciate, differentiate, special, commercial, electrician, politician, tuition, nation, negotiate na kadhaalika.
(Kumbuka kuwa inabidi ujitahidi kutafuta masomo rasmi ya namna ya kusoma matamshi, kwani hapa ni jitihada tu ya kukusaidia ingawa kwa kweli hakuna kanuni rasmi ya kutamka maneno ya Kiingereza, sio kuwa kila uliloliona humu ndio basi umemaliza.)
Katika Kiingereza herufi "g" ina namna mbili za kusomwa, namna ya kwanza husomwa kama "j" na namna ya pili kama "g"
Mfano wa namna inayosomwa kama "j"
Message, page, package, usage, passage, cartridge, porridge, hostage, wastage, lodge, budge, edge, pledge, breakage. knowledge, dodge, homage, sausage, courage,.
Yale yanayosomwa kama "G' ni
Gear, glimpse, Glance, Gauze, congratulate, English, Anglophobe, garage, carriage, usage, drainage, engage, pig, jug, thug, big, mug, hug, rug, shaggy, egg, leg, bag, tag, beg, dig, fig, figure, wig, zigzag, log, frog, fog na kadhaalika na kadhaalika. (kwa ufupi tu ujue kila neno ambalo herufi "g" katika lugha ya Kiingereza
Pia yapo maneno yaliyo ishia na herufi tatu ambazo ni "....ise", "..ice" na " ..ize".
Herufi hizi zitasomwa kama "aiz" na mahali pengine kama "ais" kwa matamshi ya Kiswahili. Tazama mfano wa maneno hayo na uyasome kwa sauti. (maneno yanayo ishia na '..ice" ndiyo husomwa kwa kutamkwa kama "ais"
standardize, personalize, minimize, sacrifice, categorize, recognized, emphasize, specialize, monopolize, ice, dice, thrice, twice, rice, surprise, sunrise, apologize,
Kwa kawaida katika Kiingereza kuna baadhi ya herufi ambazo labda msomaji wa Kiswahili aweza kupata shida kidogo katika kuzisoma, mfano wa herufi mojawapo ni "ph" Hii husimama mahali pa matamshi ya herufi "f"
maneno hayo ni kama vile Physics, pharmacy, phenomena, phone, phantom, peripheral, emphasize, amphibian, phenomenology, elephant, phony, phonate, Anglophobe, phenol.
Namna ya kuandika Kiingereza na Kutamka:
Jina lolote la kiingereza lililo na umoja na wingi,
huongezewa
- 's mwishoni kwa ajili ya kuthibitisha wingi wake, mfano: car (kaa) wingi wake ni cars (kaaz) (yaani magari)
Goat (got) maana yake mbuzi (mmoja) wakiwa wengi utaongezea s" na itasomeka kama (goats) (gots)
Kwa majina yaishiayo na 'y' yakiwa yemefuatiwa na konsonanti nyuma yake mfano "bakery" "salary" "strawberry"
"enemy" "baby" "bunny" "puppy" yote haya huondolewa heruti ya mwisho ("Y) na kuwekwa sehemu iliyoondolewa herufi tatu, nazo ni "-ies" kwa maana hiyo basi. maneno hayo hapo juu wingi wake utakuwa unaandikwa kama ifuatavyo:
UMOJA WINGI
"Bakery" (Bekari/ sehemu ya kuoka mikate) Bakeries (bekariz)
"Salary" (salare /mshahara) Salaries (salariz)
Strawberry (strobari/ tunda nyanya) Strawberries. (strobariz)
"Enemy" (enemi/ adui) enemies (enemiz)
"Baby" (beibi/ mtoto) babies (beibiz)
"Bunny" (bani / mtoto wa sungura) bunnies (baniz)
"Puppy" (papi / mtoto wa mbwa) puppies.(papiz)
"Pony" (poni/ mnyama fulani aina ya punda) ponies.
WINGI KATIKA MAJINA YAISHIAYO NA "sh" "x" "ss" "z" "ch"
Kwa kawaida majina ya vitu vinavyo hesabika yanayoishia na herufi zilizo tajwa hapo juu, yakiwa katika hali ya wingi huongezewa herufi mbili bila kuondolewa herufi yoyote za mwhisho katika herufi zake. herufi zinazoongezwa ni "es" na kutamkwa kwake ni kwa kutajwa wazi "e" "na 's" . kwa mfano : lioness itakapoongezewa wingi na kuwa " lioness" ambayo hutamkwa kama "layoneses"
mfano wa majina ya vitu hivyo ni
UMOJA (matamshi yake) WINGI
Bush (bush) bushes (bushes)
Brush ( brash) brushes .(brashes)
Box (boks) boxes. (bokses)
Princess (prinses) princesses. (prinseses)
Branch (branch) branches (branches).
NAMNA YA KUANDIKA NA KUTAMKA KWA JINA LINAOISHIA NA "O" LIKIWA KAIKA WINGI.
Upo utaratibu wa kuandika wingi katika jina lililoishia na irabu "o". Hili hutamkwa kwa kuongezewa herufi mbili yaani "es" mwishoni bila kuondolewa kwa herufi yoyote wakati wa kuandika herufi hizi mbili. hapa nitatoa mifano michache tu.
UMOJA WINGI
Mango (mengo) mangoes
Mosquito (moskwito) mosquitoes
Tomato (tomato) tomatoes.
Potato (poteito) potatoes
Hapa yabidi tuwe waangalifu maan yake sio kila jina litakalokuwa limeishia na herufi hii litaongezewa "es" likiwa katika wingi, hapa ni kwa yale majina yaliyo na asili kabisa ya Kiingreza na yamekubalika kupewa kanuni hii, kwani yapo maneno mengine yamekopwa katika lugha mbalimbali, mfano Kijapani tuna neno "kimono" na katika lugha nyingine tuna maneno kama "piano" .maneno kama haya hayatachukua kanuni hii bali yataongezewa tu "S" mw2ishoni kama yalivyo.
Mfano:
UMOJA WINGI
Kimono kimonos
Piano pianos
Bongo bongos
N.B Ikumbukwe hapo juu kuwa maneno kama
"boy" "toy" "key" n.k yanaishia na "y" lakini hayatakuwa na sheria ya kuondolewa "Y" na kuingizwa "ies"
kwa kuwa yenyewe yamekosa hali moja miongoni mwa tulizozitaja, "y" iliyopo mwishoni haikufuatiwa na konsonanti bali imefuatiwa na irabu (a, e, i, o, u)
Kwa maana hiyo basi
Boy wingi wake utakuwa ni "boys"
Toy wingi wake utakuwa ni "toys"
Key wingi wake utakuwa ni "keys"
Maneno yenye wingi unaogeuza katikati ya neno: yapo majina ya Kiingereza ambayo yakiwa katika wingi hubadilisha katikati ya neno hilo kabisa: angalia mfano wa maneno hayo hapo chini:
Jina linavyotamkwa Maana yake Wingi wake
Tooth (tuuth) Jino teeth
Goose (guuz) bata maji geese.
Mouse (maus) panya mice.
Louse (lusi) chawa lice.
nategemea kuwa hadi hapa nitakuwa kwa kiasi fulani nimeeleweka na ninataraji kuendelea baadaye tukijaaliwa katika kuendeleza hapa tulipofikia juu ya wingi na umoja, lakini hadi hapa msomaji akitumia kanuni hizi natumaini zitaweza kumsaidia kwa kiasi kikubwa sana.
MAJINA YA VITU MBALIMBALI KATIKA LUGHA YA KIINGEREZA:
Katika lugha ya Kiingereza tuanza kutaja matunda yale ambayo yanapatikana katika mazingira ya hapa Afrika:
JINA MAANA MATAMSHI
A mango embe (mengo)
A guava pera (juva)
A papaya/ a pawpaw papai (papaya/popo)
A cashew apple bibo. (Keshiu epo)
A custard apple tope tope (kastad epo)
An avocado or ("evokado" au " eligeta epo")
( alligator apple) parachichi
A melon tikiti maji. (melon)
An orange chungwa. (orenj )
A tangerine chenza. (tenjirin)
A baobab fruit ubuyu.
A tamarind ukwaju.
A date tende.
An apple epo.
A strawberry
(tunda nyanya/ (jamii ya tunda damu) tazama picha hapo juu)
A jackfruit fenesi.
A banana ndizi.
A jujube fruit tunda la mkunazi.
An olive Zeituni.
An apricot mishmish.
A pear peaz
A grapefruit balungi/dalansi.
A damson Zambarau.
A lime ndimu.
A breadfruit shokishoki.
A plum bungo.
grapes zabibu.
A nutmeg kungumanga.
A pomegranate komamanga.
Mulberry forosadi
Cucumber tango.
BAADHI YA MAJINA YA WANYAMA WA NYUMBANI KWA KIINGEREZA.
(SOME OF DOMESTIC ANIMALS' ENGLISH -SWAHILI NAMES )
A cow ng'ombe.
A goat mbuzi.
A dog mbwa.
A pig nguruwe.
A hen kuku.
A duck bata.
A donkey punda.
A guinea fowl kanga.
A dove njiwa.
A camel ngamia.
A horse farasi.
A sheep kondoo.
A cat paka.
A rabbit Sungura
BAADHI YA MAJINA YA WANYAMA WA PORINI NA MAJINI
(SOME OF SEA AND WILD ANIMALS' NAMES)
Beast mnyama yeyote aliye na miguu minne huitwa "beast" (Kwa ujumla)
Biped mnyama yeyoye mwenye miguu miwili tu huitwa "Biped"
Amphibians mnyama awezaye kuishi majini na nchi kavu: mathalan Chura n.k
A bear dubu.
An ass mnyama jamii ya farasi mwenye masikio marefu na mwishoni mwa mkiawe analo fungu
la manyoya mwishoni mwa mkia (turft) kama alivyo nalo ng'ombe.
An elephant tembo.
An ostrich mbuni.
A lion simba.
A zebra pundamilia.
A rhino kifaru.
A giraffe twiga.
A crocodile mamba.
A squirrel kicheche.
A mongoose sili.
A leopard Chui.
A cheetah duma
A monkey kima.
A gorilla sokwe.
A hippopotamus kiboko.
A hyena fisi.
A chameleon kinyonga.
A lizard mjusi.
A buffalo nyati.
A fish samaki.
A frog chura.
A snake nyoka.
A rat panya (wa nyumbani).
A flamingo kongoni.
A crane korongo
A crow kunguru.
A parrot kasuku.
A peacock tausi.
A turkey bata mzinga.
An eagle tai.
A kiwi ndege John
An octopus pweza.
A dove/ pigeon njiwa
A kite ( a bird of prey) mwewe
Antelope swala.
Baboon nyani mkubwa mwenye uso kama wa mbwa.
Badger mnyama mdogo aliye na rangi ya kijivu aishiye shimoni na anatoka usiku.
Swan aina fulani ya mabata maji.
A crab kaa.
Pony mnyama fulani jamii ya punda.
Gazelle mnyama jamii ya swala mwenye pembe ndefu zilizo jikunja.
Foal farasi mdogo.
Shark papa.
Cuttle-fish samaki wa maji ya bahari ambaye anaposhambulia hutema maji maji meusi, ngisi
Wart-hog ngiri.
A hare sungura (mkubwa wa porini)
A mule nyumbu
A whale nyangumi.
An Owl bundi.
Python chatu.
wildebeest Kongoni, nyumbu.
Wild dog mbwa mwitu.
Lobster kamba. (samaki)
Cobra
BAADHI YA MAJINA YA WADUDU KWA LUGHA YA KIINGEREZA.
(SOME OF INSECTS' NAMES)
A housefly inzi.
An ant siafu, sisimizi.
A mosquito mbu.
A louse chawa.
A cockroach mende
A bee nyuki
A spider buibui.
A centipede tandu.
A millipede jongoo.
A hornet nyigu.
A grasshopper panzi.
A tsetse fly mbung’o.
A butterfly kipepeo.
A snail konokono
Cicada
Beetle mdudu fulani anayesukuma mbolea ya ng'ombe baada ya kuitengeneza katika umbo la mpira.
Cock chaffer
Gad fly aina ya wadudu wanaowang'ata ng'ombe na farasi.
Flea kiroboto.
BAADHI YA MAJINA YA VIUNGO VYA CHAKULA:
(SOME OF SPICES' NAME)
A garlic kitunguu swaumu.
A tomato nyanya.
An onion kitunguu.
Cinnamon mdalasini.
An averrhoa mbirimbi.
An okra bamia.
(Lady finger )
A brinjal bilinganya.
An aubergine nyanya mti.
A coconut nazi.
A ginger tangawizi.
Cooking oil mafuta ya kupikia.
A pepper pilipili.
Greens mboga za majani.
Clove karafuu.
carrot karoti.
Cardamom iliki.
Caraway
Capsicum
Cayenne
Curry powder bizari.
Cabbage kabichi.
Salt chumvi.
MAJINA YA BAADHI YA VIFAA VYA JIKONI.
( SOME OF DOMESTIC (KITCHEN) UTENSILS)
A charcoal stove Jiko la mkaa.
A kerosene stove Jiko la mafuta ya taa.
A sauce pan sufuria.
A plate sahani.
A glass gilasi
A mug kikombe kikubwa.
A cup kikombe cha chai.
A spoon kijiko.
A wooden spoon mwiko.
A bowl bakuli.
A tub beseni.
A frying pan kikaango cha chapatti.
A funnel kifaa cha kupitishia majimaji ndani
ya chupa bila kumwaga chenye mdomo
mpana kwa juu na chini ni mrija ambao
huzamishwa kwenye chupa au kitu kama hicho ; chirizo.
A sieve Chujio (La chai au nazi)
A bucket ndoo.
A fork uma wa kulia chakula.
A bottle chupa.
A potato masher kifaa cha kupondea viazi vilivyo pikwa.
A kettle birika.
A jug jagi.
A ladle upawa.
A spatula kijiko cha kuopolea maadazi au samaki
kikaangoni (A fish slice kwa kiingreza cha British).
A pair of tongs kibanio ( cha kuepulia sufuria motoni au kushikilia)
Cauldron Sufuria kubwa la kuchemshia vitu.
Casserole Sufuria la kupikia na kuhifadhia joto lenye mfuniko wake maalum.
Chaffing dish dishi lenye "heater" (kichemsho) chini yake linalotumika katika meza kwa kupika na
kuhifadhi joto la chakula hicho.
Cullender, colander bakuli/dishi /chombo chenye vitobo vingi kwa ajili ya kupitisha maji kutoka kutoka kwenye
mboga n.k (Chungio)
MILO
Breakfast Istiftaah (yaani mlo wa kwanza kabisa tangu mtu aamke/kifungua kinywa.)
Brunch Mlo ambao sio wa "breakfast" wala "lunch"
Lunch Chakula cha mchana.
Dinner Chakula cha jioni.
Supper Chakula cha usiku.
BAADHI YA MAJINA YA VIFAA VINGINE VYA NYUMBANI
(SOME OF OTHER DOMESTIC TOOLS AND EQUIPMENTS)
A ladder ngazi.
A spade beleshi (chepeo)
A hammer nyundo.
A hoe jembe.
A rake reki.(kifaa kama chanuo kwa ajili ya kutoa taka taka)
An iron pasi.
A wheel barrow toroli.
A saw msumeno.
A chisel patasi.
A file msasa wa chuma.
A scissor mkasi.
A tape measure futi.
A pliers koleo.
An axe shoka.
A brush brashi.
A knife kisu,
A plane randa.
Pliers koleo.
Claw hammer nyundo yenye pembe mbili juu kwa ajili ya kung'olea misumari.
BAADHI YA MAJINA YA VYAKULA
(SOME OF FOOD STUFF'S NAMES)
Maize mahindi.
Wheat ngano.
Millet mtama.
Cassava muhogo.
Banana ndizi.
Pumpkin boga.
Beans maharagwe.
Rice mchele.
Lentils njegere.
Potato kiazi.
Irish potato mbatata (kiazi mbatata)
Sweet potato Kiazi kitamu.
Coco yams magimbi.
Yams viazi vikuu.
an egg yai.
Flour unga.
Maize flour unga wa mahindi.
Wheat flour unga wa ngano
pigeon peas mbaazi.
Barley shayiri
Oats
Rye
VIBURUDISHO (REFRESHMENTS:)
Ground nuts karanga.
A sweet pipi, peremende.
A biscuit biskuti.
A bun andazi (tamu)
Cold drinks vinywaji baridi.
Soft drinks vinywaji tulivu.
Chewing gum kitu cha kutafuna chenye ladha ya sukari kama
vile tunavyoona vile vinavyotengenezwa na viwanda
kama BIG G, Bubblish n.k.
Yoghurt mtindi.
grilled meat nyama choma.
Buttermilk maziwa ya mtindi
Copra mbata.
Butter siagi.
Cheese jibini.
Cashew nut korosho.
Cocoa kakao.
Coffee kahawa.
Tobacco tumbaku.
Popcorn bisi.
Juice maji ya matunda.
Tea (char) chai.
Hali ya dunia
Wind upepo
Typhoon kimbunga.
Earthquake tetemeko la ardhi.
Flood mafuriko.
Rain kunyesha (Mvua)
SEHEMU ZA MWILI WA BINAADAMU (Some of parts of a human being's body)
Head kichwa.
Hair nywele.
Shoulder bega.
Stomach tumbo.
knee goti.
Toe kidole cha mguuni
Finger kidole cha mkono.
Ear sikio.
Eye jicho.
Mouth mdomo.
Lip sehemu ya chini au ya juu inayo funga mdomo.
Upper lip sehemu ya juu ya mdomo inayoufunga mdomo.
Lower lip sehemu ya chini ya mdomo inayoufunga mdomo.
Throat Koo.
Nape sehemu ya nyuma ya shingo (Juu ya mgongo)
Adam's apple sehemu kwenye koo la mwanaume palipo tokeza juu na hushuka chini anapomeza kitu.
Nose pua.
Tooth jino.
Tongue ulimi.
Palate paa la mdomo.
Eyes brows nyusi.
Eyelashes kope.
Beards ndevu.
Moustache mustachi.
Bald kipara.
Fore head utosi.
Chin kidevu.
Palm kiganja cha mkono.
Ankle kifundo cha mguu.
Eye lid mstari unaopita kati ya jicho na shavu.
Temple
Cheek shavu.
Nail kucha.
Back mgongo.
Buttock makalio.(sehemu unayoikalia/uliyoikalia kama umekaa.)
Chest kifua.
Navel or
(belly button) kitovu.
Nipple sehemu kama kipele kwenye kifua chako juu ya sehemu iliyoinuka (kiziwa)
Thigh paja
Foot mguu.
Sole nyayo.
Hand mkono (sehemu ya kushikia kitu) kuanzia kwenye kiwiko hadi kwenye vidole.
Wrist kiwiko. (viungio vya "hand" na "arm"
Arm sehemu ya mkono kuanzia mabegani hadi kwenye hand.
Breast matiti.
Waist Kiuno.
Elbow Sehemu mikono yapo inapo kunjika kutoka kwenye mabega yako ukishika kiuno, kiwiko; (kipepsi),
Heel kisigino.
Skin ngozi.
Lung pafu.
Jaws taya.
MAJINA YA BAADHI YA MAVAZI. (NGUO)
(SOME OF NAMES OF DIFFERENT ROBES and other wears)
shirt shati
short kaptula
Trousers Suruali
Tie tai.
Jacket jaketi
Coat koti
Hat kofia.
pullover sweta.
T shirt fulana
Skirt sket
Blouse blauz
Surplice kanzu.
Vest fulana isiyo na mikono mirefu ivaliwayo na wanaume kabla ya kuvaa shati; kizibao.
Turban kilemba.
Socks soksi
Stocking soksi ndefu.
Veil baibui.
Jacket jaketi
Mantle
Boot viatu virefu vinavyofunika hadi vifundoni, buti.
Sandal viatu vya wazi ambavyo mara nyingi hutengenezwa kwa ngozi za wanyama; sando.
Slippers Viatuvya wazi kwa ajili ya kuogea au kwenda msalani; kandambili,
Belt mkanda.
Stocking soksi ndefu.
Socks socks fupi
Boots viatu virefu
Slippers kandambili.
Turban Kilemba
Sandal sando
Scarf nguo yenye sura ya kitambaa kizito kidogo inayozungushiwa shingoni mwa mvaaji.
Cloak
Pajamas Suruali ya kulalia.
Beach comber kaptula ambayo haijapindwa yenye nyuzinyuzi nyingi sehemu ya mwishoni kwenye miguu.
Siku za wiki (Days of a week)
Monday Jumatatu
Tuesday Jumanne.
Wednesday Jumatano
Thursday Alkhamisi
Friday Ijumaa
Saturday Jumamosi
Sunday Jumapili.
Rangi mbalimbali (Colors)
White nyeupe.
Black nyeusi
Red nyekundu.
Blue bluu.
Green kijani
Maroon damu ya mzee.
Brown kahawia
Grey rangi ya kijivu.(rangi ya simenti)
Purple rangi ya zambarao.
Yellow njano.
Yellow green
Wheat rangi ya ngano.(sio njano moja kwa moja ila imefifia)
Turquoise
Violet
Tomato rangi ya nyanya (nyekundu iliyo fifia kidogo)
Kuhesabu (Counting)
One 1 (moja)
Two 2 (mbili)
Three 3 (tatu)
Four 4 (nne)
Five 5 (tano)
Six 6 (sita)
Seven 7 (saba)
Eight 8 (nane)
Nine 9 (tisa)
Ten 10 (kumi)
Eleven 11 (kumi na moja)
Twelve 12 (kumi na mbili)
Thirteen 13 (kumi na tatu)
Fourteen 14 (kumi na nne)
Fifteen 15 (kumi na tano)
Sixteen 16 (kumi na sita)
Seventeen 17 (kumi na saba)
Eighteen 18 (kumi na nane)
Nineteen 19 (kumi na tisa)
Twenty 20 (ishirini)
Twenty-one 21 (ishirini na moja)
Twenty-two 22 (ishirini na mbili)
Twenty-three 23 (ishirini na tatu)
Twenty-four 24 (ishirini na nne)
Twenty-five 25 (ishirini na tano)
Twenty-six 26 (ishirini na sita)
Twenty-seven 27 (ishirini na saba)
Twenty-eight 28 (ishirini na nane)
Twenty-nine 29 (ishirini na tisa)
Thirty 30 (thelathini)
Thirty-one 31 (thelathini na moja)
Forty 40 (Arobaini)
Fifty 50 (khamsini)
Sixty 60 (sitini)
Seventy 70 (sabini)
Eighty 80 (themanini)
Ninety 90 (Tisini)
Hundred 100 (Mia)
Hundred and ten 110 (Mia na kumi)
Two hundreds 200 (Mia mbili)
Three hundreds 300 (Mia tatu)
Thousand 1000 (Elfu moja)
Thousand and hundred 1100 (elfu na mia)
Ten thousands 10,000 (Elfu kumi)
One million 1,000,000 (milioni moja)
Baadhi ya vyumba na majengo ya umma (Some of Public rooms and buildings:)
Hotel nyumba kwa ajili ya wasafiri yenye huduma ya mavazi na chakula kwa malipo.
Hostel nyumba kwa ajili ya wanafunzi au vikundi vinavyokodi nyumba hizo kwa ajili ya kukaa kwa mafunzo
maalum, na nyumba hizi hulipiwa chakula na malazi kwa bili.
Motel hotel yenye huduma ya kuegesha magari
Restaurant nyumba ya kibiashara inayotoa huduma ya chakula na vinywaji na yenye sehemu ya kulia chakula hicho.
Cafeteria
Cafe
Bistro ni restaurant ndogo na yenye chakula bei nafuu (mama nitilie)
Canteen mkahawa katika sehemu ya kazi au shule.
Pub nyumba inapouziwa pombe lakini haitoi huduma ya malazi wala chakula.
Inn nyumba ambayo hutoa huduma ya vinywaji, chakula na malazi humo kwa kulipiwa, (Ni tofauti na hotel)
Bar/ale house Nyumba panapouzwa pombe za aina mbalimbali na yenye sehemu za kunywea pombe hizo
za madaraja tofauti.
Grocery nyumba inayouzwa vinywaji na vyakula mbalimbali vya makopo, pakiti n.k kwa rejareja na
vilevile huuzwa baadhi ya vifaa vidogovidogo vya nyumbani.
Guest house. nyumba ya kulala wageni.
Lodging house nyumba inayotoa huduma ya malazi baada ya mtu kupokelewa kama mgeni (tazama guest house)
Boarding house nyumba itoayo huduma ya chakula (na mara nyingi hulipwa kwa bili)
Casino kasino
School shule.
College Chuo.
Market Soko.
Court korti (mahakama)
Toilet Chooni.
Shop Duka
Cinema holy Ukumbi wa sinema.
Mosque msikiti.
Church kanisa.
Pagoda nyumba ya ibada ya wapagani.
Temple nyumba ya ibada ya mabaniyani.
Doss house nyumba ya lodging yenye bei nafuu.
MAGONJWA (DISEASES )
bilharzias kichocho.
Malaria maleria
Yellow fever homa ya manjano.
Elephantiasis matende.
Shingle mkanda wa jeshi.
Acne chunusi.
Catalepsy
Beriberi beriberi.
Asthma pumu
Typhoid homa ya matumbo.
Angina pec- torsi
Anthrax kimeta.
Cholera kipindupindu.
Small pox ndui.
hernia ngiri (mshipa)
Hiccup kwikwi.
Tunakuomba ndugu msomaji utoe maoni yako juu ya website hii ambayo bado ipo katika kuendelezwa, toa maoni yako, ikosoe, tuma e mail katika anuani yangu canoksan@yahoo.com au hilalshukri@yahoo.com na waweza pia kunipa maana fupi ya baadhi ya maneno ambayo nimeshindwa kuyajua kiswahili chake.
Uionayo hapa chini ni kamusi ambayo hadi sasa hatujaikamilisha kuitengeneza, hizo ni kamusi mbili (yaani Kiingereza kwa Kiswahili na Kiswahili kwa kiingereza, Kwa maana hiyo basi hadi sasa hazipo hewani, samahani sana kwa usumbufu.